October 28, 2018


Mshambuliaji wa Simba, Emanuel Okwi ameanza kutakata baada ya kufanikiwa kufunga mabao matatu katika mchezo wake wa leo dhidi ya Ruvu Shooting na kuweza kuandika rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kufunga 'Hat-trick'.

Mchezaji wa kwanza msimu huu alikuwa ni Alex Kitenge wa Stand United ambaye alifanya hivyo katika mchezo wake dhidi ya Yanga na amekuwa hana bahati kwani mpaka sasa hajafunga bao lingine katika michezo aliyocheza.

Okwi alikuwa mfungaji bora msimu uliopita akifunga jumla ya mabao 20 alianza msimu kwa ukame wa mabao, ila ameanza kureja baada ya kufanikiwa kufikisha mabao 7 mpaka sasa kwenye ligi sawa na Eliud Ambokile wa Mbeya City.

Simba wanafakiwa kushinda kwa mara ya pili kwa ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting, ikumbukwe pia msimu uliopita Okwi aliwafunga "Hat-trick' Ruvu Shooting. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic