October 28, 2018





FC Barcelona imeitwanga Real Madrid kwa mabao 5-1 katika mechi ya La Liga maarufu kama El Clasico.

Barcelona iliyokuwa nyumbani Camp Nou, imeshinda kwa mabao hayo matano huku mshambuliaji wake kutoka Uruguay, Luis Suarez akipiga hat trick.




Mechi hiyo ilionekana mapema kuwa ya Barcelona baada ya Coutinho kuanza kufunga kabla ya Suarez kuongeza bao la pili.

Lakini Madrid walianza kipindi cha pili kwa kasi kupata bao la mapema kupitia Marcelo lakini ikawa kama wameichokoza Barcelona ambayo ilianza kufunga mfululizo, Suarez akifunga mabao mengine mawili na mkongwe, Artulo Vidal akifunga dakika chache baada ya kuingia uwanjani.



El Clasico hiyo ilikuwa maarufu zaidi kwa maana ya kuwakosa nyota wawili, Cristiano Ronaldo aliyehamia Juventus na Lionel Messi ambaye ni majeruhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic