Mchezo kati ya Ruvu Shooting Umemalizika muda huu uwanja wa taifa ulianza saa 1:00 Usiku, mshambuliaji Emmanuel Okwi anaandika bao la kwanza dakika ya 7 akipokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.
Dakika ya 23 Simba wanapata bao la 2 linalofungwa na Meddie Kagere baada ya Shiza Kichuya kupiga kona iliyogonga mwamba ikakutana na Kagere akafunga bao la 2.
Claytous Chama anamtengenezea pasi nzuri Emmanuel Okwi anandika bao la tatu dakika ya 56.
Emmanuel Okwi anapokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe dakika ya 78 na kuandika bao la nne.
Adam Salamba anaandika bao la tano akipokea pasi kutoka kwa Hassan Dilunga dakika ya 89.
Ruvu Shooting 0-5 Simba, dk ya 90 Uwanja wa Taifa.
This is SIMBAAAAAAAAA
ReplyDeleteKaz nzur xana kikubwa wajiandae kisaikolojia yanga
ReplyDeleteKaz nzur xana kikubwa wajiandae kisaikolojia yanga
ReplyDeletesiku hizi mnaripoti mechi kama hamtaki,bora muache kuliko kutuzuga kipumbavu hivi
ReplyDelete