October 27, 2018

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya England and Tottenham Dele Alli, 22 anakaribia kusaini mkataba mpya klabu hapo. (Sky Sports).
Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, 31, amemkasirikia Meneja wake Claude Puel,ambaye anadaiwa kuwa alimuondoa kutomjumuisha mchezaji huyo katika mchezo leo jumamosi dhidi ya West Ham. (Telegraph).
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaweza kupigwa faini na klabu yao baada ya kukataa kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na mfadhili wao ya kuandamana dhidi ya tatizo la usafiri ambao timu iliwahi kukabiliana nao katika mashindano ya ligi. (Mail).


Wakati huohuo Bosi wa United Jose Mourinho anataka wachezaji wake wajumuike naye kutembea kutoka Hotelini mpaka Uwanjani Old Traford kukwepa foleni inayoweza kutokea kama ilivyotokea kwenye mchezo dhidi ya Juventus kwenye UEFA ingawa watu wa usalama nchini humo wamepinga zoezi hilo. (Mail).
Tottenham imepanga kumsainisha mchezaji wa Brazil Malcom, 21,wa Barcelona ambaye anahangaikia kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho na Ousmane Dembele. (Corriere dello Sport - in Spanish).
Kiungo wa kati Mousa Dembele, 31 yuko katika orodha ya juu ya wachezaji wa Tottenham ambao meneja Mauricio Pochettino anataka kuwauza katika kipindi hiki cha kiangazi. (Sun).
Kiungo Aaron Ramsey, 27,amejiudhuru ili aondoke timu ya Arsenal katika kipindi cha kiangazi, ingawa amesema kuwa anashangaa kwanini Arsenal wamesitisha tena mkataba wake wa miaka minne (Evening Standard).
Bosi wa Newcastle Rafael Benitez, anaweza kuwa nje ya mkataba katika kipindi cha kiangazi, hivyo amependekeza kuwa anaweza kuiongoza timu katika msimu ujao licha ya kuwa timu hiyo iko katika kiwango cha chini katika ligi za Premia. (Mirror).
Je Benitez ataondoka? klabu ya Newcastle inatarajia kumchukua meneja wa zamani wa Monaco Leonardo Jardim licha ya kuwa Meneja huyo anavutiwa na Leicester. (le10sport - in French).
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, alisikitishwa kwa kutoitwa katika kikosi cha England kilichoenda kwenye kombe la dunia hivyo amekata tamaa kuichezea tena nchi yake. (Telegraph, subscription required).
Mlinda Mlango wa Burnley na timu ya taifa ya England Joe Hart, 31, ameweka wazi namna alivyoumia alipoachwa kwenda kombe la dunia, ambapo aliamua hata kujiondoa kwenye kundi la WhatsApp la timu hiyo..
Klabu ya Manchester United bado imeendelea kuwa na mipango ya kumsaninisha beki wa pembeni raia wa Hispania Jordi Alba, 29, kwenye dirisha la usajili la mwezi January ambapo itachukua mpaka mwisho wa msimu kwa Fc Barcelona kumuongeza mkataba mpya beki huyo (Diario Sport - in Spanish).
Meneja Jose Mourinho amethibitisha kuwa Manchester United haitamsajili tena mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo ambaye pia ni raia wa Swedini Zlatan Ibrahimovic, 37, anayechezea klabu ya Los Angeles Galaxy. (Manchester Evening News).
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amesema Mourinho atarudi kufundisha klabu hiyo kama kocha inaweza kuwa 'kipindi hiki au baadae' (ESPN).
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya England Ruben Loftus-Cheek, 22, amesema amegairi kutoka nje ya Chelsea kwa mkopo kwani anahitaj aendelea kujifunza kutoka kwa Maurizio Sarri. (Evening Standard).
Paris St-Germain imepanga kumsajili beki wa West Ham Issa Diop, 21, na kumpa kitita cha pauni £50m. (Mail).
West Ham italazimika kutumia hadi pauni milioni 33 kumsajili kiungo wa Paraguay Miguel Almiron, 24, kutoka klabu ya Atlanta United. (Ultima Hora - in Spanish).
Klabu ya Bayern Munich ameungana na Manchester United katika mbio za kuwania saini ya beki wa Fiorentina Nikola Milenkovic, 21. Ingawa imethibitishwa kuwa mlinzi huyo raia wa Serbia hauzwi chini ya pauni milioni 50. (Calciomercato - in Italian).
Vilabu vikubwa barani Ulaya vipo katika majadiliano ya namna ya kuthibiti ongezeko kubwa la wachezaji wanaodai mishahara mikubwa, ambapo hofu hii imeongezeka kwa kasi ya ajabu, hivi sasa mishahara inaongezeka bila hata udhibiti wa vilabu husika (Sun).
Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic