Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameshindwa kuzuia hisia zake na kusema kuwa timu imepata kiungo mkabaji raia wa Zambia, Claytous Chama na kumpa onyo kali.
Aussems alisema kuwa Chama ni moja kati ya wachezaji wenye vipaji Afrika, anaamini ni hazina kubwa kwa nchi yake ya Zambia kwa siku za baadaye hivyo hatakiwi kubweteka.
"Huyu kijana ana kipaji cha hali ya juu ni hazina kwa taifa lake ninamshauri asibweteke azidi kujituma ni suala la muda tu kwake aweze kucheza kimataifa na kudumisha nidhamu kwani hicho ndicho huwashinda wachezaji wengi," alisema.
Chama alijiunga na Simba msimu huu akitokea timu ya Power Dyanamo ya Zambia, mpaka sasa ametengeneza pasi moja ya bao, amefunga mabao mawili dhidi ya Stand United na Alliance FC, kesho atakuwa na kibarua mbele ya Ruvu Shooting.
Chama ni kiungo mshambuliaji na aio kiungo mkabaji. Msipotoshe.
ReplyDelete