October 7, 2018


Kuelekea mechi ya leo baina ya Yanga na Mbao FC, Kocha Amri Said 'Stam' ametamba kuwoanjesha wapinzani wake joto la jiwe.

Stam ameeeleza kuwa maandalizi yao yalikuwa moto kuelekea mechi hiyo inayopigwa leo majira ya saa 1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo amesema watapigana kufa na kupona kuhakikisha wanachukua alama 3 za Yanga ili kuendelea kujitengenezea nafasi ya kuwa juu kwenye msimamo wa ligi.

Mbao wameonesha dhamira ya kuifunga Yanga ili kuhakikisha wanaweka historia ya kuzifunga timu hizo kongwe ikiwemo Simba ambayo waliifunga CCM Kirumba, Mwanza.

Upande wa Yanga nao wametoa tahadhari kwa Mbao wakiwaambia wasidhanie kuwa wanenda kucheza na Simba kwani hakutakuwa na msalia mtume.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic