RASMI 'OUT' SIMBA
Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma, hakuwepo kwenye benchi la Simba jana usiku katika mechi dhidi ya African Lyon na licha ya kwamba viongozi wamekuwa wagumu kufafanua lakini Spoti Xtra limejiridhisha kwamba biashara ya Masoud na Simba imekwisha.
Habari zinasema kwamba Masoud alikutana na muwe- kezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ juzi Ijumaa jioni na kufi kia maku-baliano ya kuvunja mkataba baada ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems kuweka wazi kwamba hayuko tayari kufanya naye kazi.
Habari zinasema kwamba Aussems amewaambia viongozi kuwa Masoud ana mambo ambayo hayawezi kuipa timu mafanikio, hivyo hawezi kuendelea kukaa naye ndani ya timu kwa madai kuwa atamvuruga.
Mmoja wa vigogo wa Simba aliyefanikisha ujio wa Masoud nchini ambaye amewahi kushikilia nafasi ya juu kwenye uongozi wa TFF enzi hizo akiwa mtumishi wa umma, juzi jioni alikwenda kambini kumshawishi Aussems lakini akamwambia ; “Hapana Masoud simtaki.”
Imejiridhisha kuwa Masoud jana alibeba kila kilicho chake kwenye kambi ya Simba iliyoko katika Hoteli ya Seascape na ameaga wachezaji na kuwatakia kila la kheri.
Masoud anatarajiwa kuondoka nchini leo au kesho kwa usafi ri wa barabara akitumia gari yake binafsi kurejea kwao Burundi.
Wewe unahakika gani kama Masoud atatumia usafiri wa barabara? Hujui kama unamuhatarishia maisha yake na majambazi? Bila hata kutumia taaluma ya habari kwa mtu mwenye upeo wake hawezi kuandika mambo ya mtu binafsi hasa unapozungumza vitu vya kufikiria.
ReplyDeleteUsikimbilie kumlaumu mwandishi tu,inawezekana ana chanzo cha habari kilichompa ruhusa kuandika habari binafsi za mtu huyo.
ReplyDeleteanmkimbia makambo
ReplyDelete