Kocha Mkuu wa Yanga, raia wa DR Congo Mwinyi Zahera, amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Lipuli FC ya Iringa hatakuwa tayri kuona anapoteza pointi mbele yao.
Mchezo wa mwisho Yanga ilikutana na KMC ambapo mchezo wao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na pointi tatu zilizoifanya kufikisha idadi ya pointi 22 na kuifanya iwe kwe nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara, nyumba ya Azam na Simba.
Akizungumza hivi karibuni Zahera alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri kuhakikisha kinapambana kuchukua pointi tatu mbele ya Lipuli, pamoja na kwamba kitaingia mchezoni huku kikiwakosa nyota wake kadhaa kama Papy Tshishimbi, Ibrahim Ajibu na Juma Mahadhi ambao wote wana majeruhi.
“Mbali na kuwakosa nyota hao pia tutamkosa Andrew Vicent ‘Dante’, ambaye naye alikuwa anaumwa lakini pia akapata adhabu ya TFF baada ya kuchezeana rafu na mchezaji wa Simba katika mchezo wetu uliopita,” alisema Zahera.
Weka akiba ya maneno mwinyi.
ReplyDelete