ALIYEIKIMBIA YANGA AOMBWA KUREJEA
Ikiwa ni siku ya pili pekee tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kwa wachezaji wa mpira hapa nchini, aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga, Geoffrey Mashiuya amesema anahitajiwa na na mabosi wake wa zamani.
Mwashiuya ambaye alisajiliwa na Yanga akitokea Kimondo FC kisha baadaye kutimkia Singida United, ameitaja Yanga kuwa ni moja ya timu ambazo zinahitaji aweze kurejea.
Mchezaji huyo ameeleza kuwa endapo Yanga watahitaji huduma yake na wakafikiana mwafaka mezani, hatokuwa na shida ya kurudi kutokana na alipo hivi sasa mambo hayaendi sawa.
Mwahisuya ameeleza mpaka sasa hajalipwa hata senti 50 ya fedha za usajili na Singida United jambo ambalo linamfanya akose hamu ya kuendelea kucheza soka lake ndani ya timu hiyo.
Ukiachana na Yanga, Mwashiuya ameitaja pia KCB ya Kenya kuhitaji huduma yake na yeye amefunguka haoni tatizo kuelekea popote ilimradi maelewano yawe mazuri.








0 COMMENTS:
Post a Comment