November 16, 2018


Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba SC, Daniel Agyei amefanikiwa kutwaa tuzo ya mlinda mlango bora katika Ligi Kuu ya Ethiopia.

Agyei ambaye anaichezea klabu ya Jimma Kenema kwa sasa, amefanikiwa kubeba tuzo hiyo katika msimu wa 2017/18.

Kipa huyo aliachwa na Simba baada ya kuonekana hana msaada wowote ndani ya wekundu hao wa Msimbazi amezidi kung'ara ndani ya klabu hiyo ambapo mpaka sasa Jimma ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Jimma ipo nyuma ya Makelle Kenema iliyo nafasi ya pili ikiwa na alama tatu huku ikiwa imecheza mechi moja pekee.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic