November 2, 2018


Beki wa timu ya Simba, Erasto Nyoni amesema anajua kuna ugumu katika kupata matokeo kwenye ligi kutokana na ushindani uliopo kwa sasa, ila sio kikwazo kwao kuendeleza ubabe.

Nyoni alikuwa nje kutokana na kupata adhabu kutoka kwa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kudaiwa kutokuwa na mchezo wa kiungwana katika mchezo wa watani wao wa jadi Yanga na kufungiwa kucheza michezo mitatu.

"Tunajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo hicho pia ni kipaumbele kikubwa kwetu na tutaonyesha juhudi kupata matokeo mbele ya wapinzani wetu  tutafanikiwa kwa kuwa tuna kikosi kipana.

"Ushirikiano uliopo ndani ya timu ni mkubwa na kila mmoja anajua wajibu wake hivyo nafasi ambayo tupo si ya kukatisha tamaa wala haitishi tuna kazi ya kutetea ubingwa hilo lipo wazi na linawezekana, sapoti kwa mashabiki muhimu," alisema.

Michezo aliyokosa ni ule dhidi ya Alliance,Stand United pamoja na Ruvu Shooting ambayo ilichezwa uwanja wa taifa na Simba ilifanikiwa kupata pointi tatu katika michezo, kesho watacheza na JKT Tanzania Uwanja wa Mkwakwaani Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic