Beki wa kushoto wa timu ya Simba, Asante Kwasi ambaye pia ni mpachika mabao kila apatapo nafasi atakosa mchezo wa kesho dhidi ya timu ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kwasi msimu uliopita alimaliza akiwa amepachika mabao 7 na ameanza vizuri pia msimu huu baada ya kufanikiwa kupachika bao moja katika mchezo wa Alliance amebaki Dar es Salaam wenzake wakiwa Tanga.
Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Kwasi ameshindwa kujiunga na wenzake kutokana na kusumbuliwa na misuli hivyo ataendelea na matibabu ili kuweza kuwa sawa.
"Wachezaji wote wapo vizuri, isipokuwa Asante Kwasi amebaki Dar kutokana na majeruhi, anasumbuliwa na misuli, ila tupo vizuri tunawaheshimu wapinzani wetu tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo," alisema.
Simba itakutana na JKT ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting walioupata jumapili ya wiki iliyopita katika ligi kuu.

0 COMMENTS:
Post a Comment