November 9, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, awamu hii amewaibukia vikali mashabiki na wanachama wa Yanga wanaotupia lawama wachezaji wake wakidai kuwa hawana kiwango kinachorodhisha, imeelezwa.

Zahera amesema kuwa wachezaji wake wanapitia wakati mgumu hivyo kwa namna wanavyopambana uwanjani hakuna haja ya kutupa lawama.

Kocha huyo ambaye yupo kwao Congo hivi sasa kwa majukumu ya timu ya taifa, amesema kuwa ni vema mashabiki wakaenda kujionea namna wachezaji hao wanavyopambana mazoezini.

Kauli hiyo imekuja kutokana na lawama kutoka kwa mashabiki kuzidi jambo ambalo limekuwa likimkera kama kocha wa timu.

Aidha, Zahera amewataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani pindi timu inapocheza ili kutoa morali ya maana kwa wachezaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV