November 6, 2018


Klabu ya Simba juzi ilimtangaza rasmi Mtendaji Mkuu (C.E.O), Crescentius Magori huku akitangaza kwamba moja ya mipango yake ambayo ataifanya baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo, ni kuhakikisha klabu hiyo inakuwa kubwa barani Afrika.

Magori ametangazwa kuwa CEO wa Simba Jumapili kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, Magori amesema kuwa haikuwa rahisi kwake kukubali kuchukua nafasi hiyo lakini mara baada ya kuteuliwa atakachokifanya ni kuifanya klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu kubwa barani Afrika.

“Haikuwa kazi rahisi kwangu kukubali jukumu hili, nilisita kwa sababu niliona ni zito. Nikaomba kuambiwa majukumu yangu pamoja na ajenda ambazo nitazifanya baada ya kupewa kazi hiyo.

“Baada ya kupewa kazi hii nitakachokifanya ni kuiandaa Simba iwe ya kisasa zaidi, nitaisimamia klabu hii na kufanya kazi nzuri kwa ajili ya wanachama mjivune na mtembee vifua mbele.

“Lakini pia nitaifanya Simba kuwa moja ya klabu kubwa barani Afrika kwa kuitoa mahali ilipo kwa sasa na kuipeleka mbele zaidi,” alisema Magori.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic