November 6, 2018


Na George Mganga

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Omar Kaya, ameibuka na kusema kuwa suala la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati yao ya Uchaguzi kutangaza kuanza mchakato wa kuwasimamia bado halijawapa nguvu ya kubadili msimamo wao.

Kaya amefunguka akieleza kinachotakiwa kufanyika ni kukutana na wanayanga wenyewe ili kulijadili hilo kabla ya kuitikia walichokisema TFF jana kupitia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ally Mchungahela.

Kaimu huyo amesema yeye hawezi kuzungumza zaidi kwa kina kutokana na Yanga si ya kwake peke yake bali ni ya wanachama, hivyo watakapokutana wataamua kipi wakifanye.

Ikumbukwe mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuitaka TFF isimamie uchaguzi wa Yanga, klabu hiyo ilikuja na kusema hawataweza kusimamiwa kwa kuwa wao wenyewe wana uhuru wa kuufanya kivyao.

BMT iliwapa maagizo TFF wakiamini Yanga haina Kamati ya Uchaguzi ambayo inajitosheleza kwa ajili ya kusimamia mchakato mzima ili kujaza nafasi za viongozi ambao nafasi zao hazina watu.

2 COMMENTS:

  1. Nanyi viongoz acheni ubabaishaji, fanyeni uchaguzi tupate viongozi timu isonge mbele

    ReplyDelete
  2. Nanyi viongoz acheni ubabaishaji, fanyeni uchaguzi tupate viongozi timu isonge mbele

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic