November 4, 2018


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali, amewaasa wanachama wa klabu hiyo kuwa makini kuelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi utakaofanyika kesho Jumapili ili kutojutia hapo baadaye.

Simba inatarajia kufanya uchaguzi mkuu kesho katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo Ocean Road jijini Dar kuanzia asubuhi hadi jioni ambapo wajumbe 18 wanagombea nafasi mbalimbali za uongozi ambazo ni za ujumbe na uenyekiti watakaokaa madarakani kwa miaka minne.

Uchaguzi wa Simba unakwenda katika mfumo wa mabadiliko kufuatia uwekezaji uliowekwa na mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ kwa kuweka kiasi cha shilingi bilioni 20 ambapo klabu hiyo itakwenda kuwa kampuni.

Dalali alisema kuwa, ni vyema wanachama wakafanya maamuzi sahihi katika uchaguzi huo ili wasije kujuta mbele ya safari.

“Uchaguzi huu ni wa kihistoria Simba inakwenda kubadili mfumo wake na inakwenda kuwa kampuni hivyo ni busara kwa wanachama kuchagua watu sahihi kulingana na kipindi kilichopo kwa kuangalia watu watakaofaa zaidi.

“Wachaguliwe watu wenye vigezo vinavyofaa katika kuingia kwenye bodi ya wakurugenzi kwa maendeleo ya Klabu ya Simba na si vinginevyo ili watu wasije wakajutia baadae,” alisema Dalali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic