November 4, 2018


Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amepinga tetesi kwamba amekuwa akimshawishi mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi, 31, kujiunga na klabu hiyo.

Tetesi zingine zinasema mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi, 25, anajiandaa kutia saini mkataba mpya na Inter Milan licha ya vilabu kadhaa vya Ulaya kummezea mate ikiwemo Chelsea, kwa mujibu wa gazeti la Calcio Mercato la Italia.

Vilevile, kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amesema klabu hiyo haitamsajili mchezaji yeyote wakati wa msimu wa uhamisho wa wachezaji mwezi Januari.  Hii ni kwa mujibu wa gazeti la Independent.

Chelsea inataka kutumia fursa ya hali ya sitofahamu ya inayoikumba Real Madrid kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ubelgiji, Eden Hazard. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27,  huenda akapewa unahodha wa timu endapo atasalia katika ligi ya premia.


Ripoti za gazeti la Telegraph zinasema kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino,  amedokeza azma yake ya kusalia katika klabu hiyo hadi atakapostaafu.

2 COMMENTS:

  1. Kuhusu kuondoka kwa messi ni kupamba Habaritu #Messi pale haondok

    ReplyDelete
  2. Afu cjaona post ya Suarez kupga bao 2 kutoka kweny 3 kaja mbili hafai fireeee ubingwaa ulee kama wote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic