November 16, 2018


Teknolojia ya VAR au ya kutumia video kutoa uamuzi itaanza kutumika katika ligi kuu ya England msimu ujao baada ya vilabu vinavoshiriki ligi hiyo kukubaliana kimsingi.

Tayari majaribio yamekuwa yakifanywa katika baadhi ya mechi za msimu huu.

Wasimamizi wa mechi za ligi hiyo wanatarajiwa kutuma ombi rasmi kwa bodi ya kimataifa ya kandanda na shirikisho la kandanda duniani FIFA.

Tayari teknolijia hiyo inatumika katika ligi za Italia na Ujerumani ili kutoa uamuzi.

Vilabu vya Arsenal na Tottenham zinamng'ang'ania mlinzi wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 24. (Daily Record)

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 29, hajaonyesha umahiri wake tangu alipojiunga na Man U.

Hii ni baada ya kiungo huyo kucheza kungia uwanjani kama mchezaji wa ziada katika derby ya Manchester sikuu ya Jumapili. (Sun)

Alexis Sanchez (kulia) aliifungia Arsenal mabao 80 baada ya kuiwakilisha mara 166 goals in 166
Klabu ya Chelsea huenda ikafungiwa kufanya usajili kwa miaka miwili ikiwa itapatikana na hatia ya kukiuka kanuni za usajili.

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limekuwa likiwachunguza The Blues kwa miaka mitatu.

Uchunguzi huu ni kuhusu kusaini wachezaji waliyo chini ya miaka 18, ikiwa ni pamoja na mchezaji wa zamani Bertrand Traoré(Football leaks)

Bayern Munich inaamini kuwa itamsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27. (Independent)

Ramsey hajahitimu kuwa kiungo kamili wa kati kwa hivyo Arsenal imlikuwa sawa kumuachilia asema Stewart Robson mchezaji wa zamani wa Gunners. (Love Sport Radio)

AC Milan inataka kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 25,mwezi Januarui mwakani. (Corriere dello Sport)

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, anaazimia kusalia Juventus,licha ya tetesi kuwa anamezea mate Manchester United. (Mirror)

Meneja mkuu wa Barcelona Pep Segura hajafutilia mbali uwezekano wa Neymar,nyota wa Brazil anaechezea klabu ya Paris St-Germain kurejea Nou Camp. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Leicester City Mhispani Vicente Iborra, 30, ana mpango wa kurejea Levante. (Super Deporte)

Iborra (kulia) alikua katika kikosi kilichoitimua Sevilla katika ligi ya mabingwa msimu uliyopita
Mshambuliaji wa Newcastle Muingereza wight Gayle, 28, anatafakari uwezekana wake wa kusalia West Brom mkatba wake wa mkopo utakapokamilika. (Birmingham Mail)

Juventus imepewa ofa ya kumsajili kipa wa Real Madrid raia wa Costa Rica Keylor Navas. (Corriere di Torino, via Mirror)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic