November 16, 2018


Uongozi wa Singida United, umejipanga kuhakikisha kwamba unaimarisha kikosi chake msimu huu hasa kupitia dirisha dogo ambalo limefunguliwa jana kwa kusajili wachezaji makini.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa klabu yake kwa sasa imeyumba kiuchumi kutokana na ukata  unaowakumba na kuwataka wadau waweze kuipa sapoti timu hiyo iliyopanda daraja msimu uliopita.

"Tutatumia dirisha dogo kufanya usajili makini na kuongeza wachezaji wapya watano kutoka klabu mbalimbali hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na Simba ili kuongeza nguvu," alisema.

Sababu kubwa ya kukumbwa na ukata ni pamoja na ligi kuu kukosa mdhamini mkuu na imeweza kuvunja mkataba na wachezaji wake akiwemo mlinda mlango Peter Manyika aliyejiunga na KCB ya Kenya.

1 COMMENTS:

  1. watu wenyewe wanashindwa kulipa mishahara wachezaji labda wategemee huruma ya Mo Dewji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic