November 2, 2018


Na George Mganga

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini, Alex Mkeyenge, amewataka Yanga kuhakikisha wanajaza nafazi zote zilizo wazi katika uchaguzi mkuu ujao.

Mapema jana Baraza la Michezo Tanzania (BMT) lilitoa maamuzi ya Yanga kuhakikisha Yanga inafanya uchaguzi ndani ya mwezi mmoja ikiwemo kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa klabu.

Mkeyenge ameeleza kuwa Yanga inapaswa kujaza nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Mwenyekiti pamoja na ya Makamu Mwenyekiti.

Kaimu huyo amesema Yanga watalazimika kujaza nafasi ya Mwenyekiti ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Yusuf Manji ambaye alitangaza kuachia ngazi.

Kiongozi huyo wa BMT amefunguka kutokana na kueleza kuwa licha ya klabu kutambua kuwa Manji bado ni Mwenyekiti wa Yanga, na kuombwa mara nyingi kurejea, hajawahi kutoa ushirikiano wowote.

Ikumbukwe Yanga imekuwa ikimuomba kila nyakati Manji ambaye mwenyewe kwa maamuzi yake binafsi aliamua kujiuzulu wadhifa huo kwa madai ya kuwa alihitaji kupumzika.

Kutokana na kutorejea kwa Manji, Mkeyenge amewataka Yanga kuhakikisha wanajaza nafasi yake na zingine tajwa hapo juu ili kutimizwa matakwa ya klabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic