NAMNA SERIKALI ILIVYOIIBUA MIGOGORO YA YANGA
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeibuka na kueleza kuwa migogoro na matatizo mbalimbali yanayoiandama klabu ya Yanga imepelekea watoe maagizo ya kuitaka ifanye uchaguzi.
Kwa mujibu wa Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa, ameeleza kuwa Yanga ilifika hatua ikaanza kutuma malalamiko yake katika ofisi ya Rais.
Aidha, Mkwawa amesema pia licha ya kufika kwa Rais, Yanga walimfuata pia Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Harrison Mwakyembe ambaye mara ya mwisho alikutana nao katika mkutano mkuu wa klabu na kuwataka wajiandae kwa kufanya uchaguzi.
Msajili huyo amesema Yanga imekuwa katika mgogoro mrefu wa kikatiba na kisheria pia katika masuala mazima ya kiutendaji, jambo ambalo limeifanya ishindwe kuhimili vishindo hivyo.
Kutokana na hayo yote kujitokeza, imefikia hatua BMT imeamua kuwataka wafanye uchaguzi ili mambo yaweze kwenda sawa ambapo wamepewa mwezi mmoja pekee.








0 COMMENTS:
Post a Comment