Imeelezwa kuwa wachezaji watano wa timu ya Singida United wameomba kuachana na timu hiyo kutokana na kile walichodai kwamba ni hali ngumu ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo.
Wachezaji hao ni pamoja na Salum Chuku, Swalehe Abdalah, Kenny Ally, Tiber John na Eliuter Mpepo.
Mmoja wa wachezaji hao amesema kuwa mambo ndani ya timu yanakwenda mdogomdogo na hajui kinachoendelea kwa sasa ndani ya timu kutokana na matatizo hayo.
"Kwa sasa sipo kambini na sijui nitakwenda lini kambini, mambo yanakwenda hivyohivyo tu kwenye timu ila kuna mambo mengi ambayo siwezi kuyaweka wazi kwa sasa," alieleza.
Katibu Mkuu Festo Sanga alisema kuwa wachezaji wote ambao wanaondoka ndani ya klabu hiyo hufuata utaratibu hivyo kuondoka kwao hakuna uhusiano na hali mbaya ya kiuchumi.
0 COMMENTS:
Post a Comment