November 16, 2018


Kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Mbambane Swallows ya Swaziland, imeelezwa wapinzani wa Simba wamejipanga kuwachunga wachezaji wake ambao taarifa zao wamezipata kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Mbabane Swallows wameeleza kupata taarifa za wachezaji kadhaa ambao ni Mzambia, Clatous Chama, Mganda, Emmanuel Okwi na Watanzania John Bocco na Erasto Nyoni kuwa nidiyo ngome ya Simba.

Taarifa imeeleza kwamba Mbambane wamepata habari za wachezaji na wanacokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanapiga tizi la maana ili kuhakikisha wanawapa wakati mgumu wa kucheza na nyavu zao.

Simba na Mbabane zitakutana kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Novemba 27-28 na mchezo wa maruadiano utafanyika huko Swaziland wiki moja baadaye.

Tayari kikosi cha Simba kimeendelea kujifua na mazoezi ya kufa mtu kwenye Uwanja wa Bocco Veterani tayari kuelekea mechi hiyo kubwa ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic