MWENYEKITI WA MATAWI YANGA ATUA KOMBORA HILI TFF KISA BAKILI MAKELE
Baada ya Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Tanzania, Bakili Makele kupigwa rungu la adhabu ya kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka mitatu, Mwenyekiti mwenza huko Zanzibar amewarushia kombora TFF.
Mwenyekiti huyo ameibuka na kueleza kuwa TFF ya sasa imekuwa ya kufungia watu pindi pale inapokosolewa na imekuwa haitaki kurekebishwa ili ifanye kazi kiueledi.
Ameeleza kuwa imekuwa ikiendeshwa kibabe chini ya Rais wake, Wallace Karia jambo ambalo lijajenga wasiwasi kwa baadhi ya viongozi wa klabu za Ligi Kuu Bara na kuondoa ile hali ya kujiamini katika kazi.
Mwenyekiti huyo amefika mbali kwa kusema kitendo cha Makele kufungiwa miaka mitatu ni cha uonevu na akieleza hakustahili kupewa adhabu hiyo ambayo anaamini haikuwa sahihi.
Makele alifungiwa na TFF kwasababu za kupinga suala la uchaguzi Yanga kufanyika huku wasimamizi wakitokea katika kamati ya shirikisho ambapo adhabu hiyo imeenda sambamba na milioni 2 za kitanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment