November 16, 2018


Kuelekea uchaguzi mkuu wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13 2019, mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Ramadhan Kampila, amesema hana wasiwasi na suala la kuchuka fomu TFF.

Mchezaj huyo naye amekuwa akipigiwa upatu wa kwenda kuchukua fomu na baadhi ya wadau wa klabu hiyo lakini mpaka sasa bado hajafika kunako shirikisho hilo wala katika makao ya klabu yake.

Licha ya kuhitajika na wadu hao badhii, Kampira amewataka wanachama wa Yanga kuendelea amani na usalama katika kipindi hiki pia kuacha migongano isiyo na msingi.

Ameeleza ni vema amani ikatawala zaidi kipindi hiki mpaka pale uchaguzi utakapowadia ili kupata uongozi mpya ambao utakuwa madarakani kwa kipindi kijacho.

Aidha, Kampira amesema haoni shida uchaguzi kusimamiwa na kamati za uchaguzi kupitia TFF na Yanga kwakuwa serikali yenyewe imeamua iwe hivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic