Maisha ni mapambano na wakati mwingine ni vizuri “raha ujipe mwenyewe”. ndio kama ambacho amekifanya mwanasoka Hulk kutoka Brazil.
Hulk ambaye aliwahi kucheza soka nchini Ureno ameamua kununua ndege yake binafsi kwa ajili ya usafiri.
Hulk amenunua ndege hiyo huku bado akiendelea kukipiga katika kikosi cha Shanghai SIPG.
Kabla ya kutua Shanghai SIPG, Hulk alikuwa akikipiga Zenit St Petersburg ambayo ilimuuza Shanghai SIPG kwa kitita cha pauni milioni 45.
Hulk ni kati ya wachezaji wanaochota mshahara mkubwa kwani kila wiki anakusanya £350,000 kutoka kwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu China maarufu kama Super League.
Ndani ya ndege hiyo, Hulk ameweka picha kadhaa zinazomuonyesha akiwa na jezi ya timu yake hiyo ya China.
0 COMMENTS:
Post a Comment