Baada ya nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu kukosekana katika mechi mbili za ligi ambazo zote timu hiyo ilishinda bao 1-0, meneja ameibuka na kuweka mambo wazi.
Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Athuman Ajibu alisema siyo kweli kwamba mteja wake ameigomea Yanga; “Mashabiki wanapaswa waache kuzusha maneno juu ya Ajibu, huo ni uzushi ambao hauna faida, ipo wazi anasumbuliwa na maumivu ya mgongo hali ambayo inamfanya awe nje kwa matibabu kwa sasa ameshatengamaa kinachosubiriwa ni ruhusa ya daktari tu acheze.”
“Kocha Zahera na Ajibu ni marafiki, hawawezi kufikia hatua hiyo, bado ana kazi ya kuonyesha uwezo ili akubalike na kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi, sasa kufikia malengo hayo ni lazima mchezaji aonekane uwanjani,” alisema Athumani ambaye amekiri Yanga wameanza mazungumzo ya mkataba na mchezaji huyo.
Ajibu amehusika katika mabao11 kati ya 6 ambayo Yanga wameshinda akitengeneza pasi nane na kufunga mabao 3.
0 COMMENTS:
Post a Comment