November 2, 2018


Tamko lilitolewa na Bodi ya Ligi Tanzania Bara jana Jumatano, linamaanisha kwamba John Bocco na wachezaji wengine wa Simba hawataiona mechi ya EPL baina ya Bournemouth na Man United itakayopigwa Jumamosi saa 9:30 alasiri.

Bodi hiyo imekataa ombi la Simba kutaka mechi yao na JKT Tanzania ichezwe kesho Ijumaa ili wajiandae kwa uchaguzi wa Jumapili Jijini Dar es Salaam. Hiyo inamaanisha kwamba Bocco wakati Man United inacheza hataweza kuwaona, Simba watakuwa wanajiandaa kushuka kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema; “Tulipokea barua ya Simba wakiomba turudishe nyuma mchezo uwe Ijumaa badala ya Jumamosi, ambapo walieleza kuwa kutokana na uchaguzi kufanyika Jumapili.

Jambo hilo kamati imeona haliingiliani na suala la mchezo, wanaocheza ni watu wengine na wanaofanya uchaguzi ni watu wengine tukawajibu kuwa ratiba itabaki vilevile, wanaweza kwenda na kurejea kufanya uchaguzi.”

Simba wanafanya uchaguzi mkuu Jumapili, katika mfumo mpya wa mabadiliko ambapo klabu hiyo inakwenda kuwa kampuni baada ya muwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’ kuweka kiasi cha Shilingi bilioni 20 akiwa na asilimia 49 na wanachama wakiwa na asilimia 51.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic