Baada ya kusajiliwa na timu ya Azam kwa kandarasi ya mwaka mmoja, mshambuliaji Obrey Chirwa amesema kuwa hesabu zake kwa sasa ni kuzifunga timu kubwa Simba na Yanga ili kuweza kukuza jina lake.
Chirwa ambaye alivunja mkataba na timu yake ya Nogotoom ya Misri kwa kushindwa kulipwa stahiki zake, amesema kuwa hata Azam FC wakimzingua atavunja mkataba.
"Mashabiki waniombee na kuniunga mkono, ninachowaza kwa sasa ni kufunga tu hasa Simba na Yanga ambazo ni timu kubwa najua nikifanya hivyo zitasaidia kufanya jina langu liwe juu," alisema.
Chirwa alitambulisha na Azam FC iliyo chini ya Hans Pluijm na kufanya awe mchezaji wa kwanza kutangazwa kabla ya dirisha dogo kufunguliwa ambapo linatarajiwa kufunguliwa 15 Novemba.
Ha ha haaaa!!!! Chirwa Bhana...unachowaza kufunga ni Yanga na Simba tuu kwa sababu ni Timu kubwa...Hizi ni timu Kongwe braza inawezekana usipate hata goli moja ukicheza nazo na Misumali wanaweza kukupiga. Alafu sasa...unawazaje Simba na Yanga tu wakati zipo timu takribani 19 zaidi ya hiyo Azam????muda huu waza kuipa mafanikio Azam na si kuwaza kuzifunga Simba na Yanga. Haya ndio mawazo ya timu ndogo zetu za Tanzania...kukaza wanapocheza na Simba na Yanga alafu wanafungwa na wasiofikirika...DuuuuuuuuuuuuHHHH!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete