Na Lunyamadzo Mlyuka
Mshambuliaji wa timu ya Mbao FC Said Khamis amesema kuwa hesabu zake kwa sasa ni kuhakikisha anafanikiwa kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ya kupachika mabao 20 msimu uliopita.
Okwi alifanikiwa kuwa mfungaji bora msimu uliopita baada ya kufunga mabao 20 ambayo yalimfanya aweze kushinda tuzo hiyo na kukabidhiwa zawadi ya shilingi Milioni tatu.
"Bado naendelea kupambana kila ninapopata nafasi na kwa sasa najua kwamba ligi inaendelea hivyo nitaendelea kufunga na ninahitaji kufunga mabao zaidi ya 20 msimu huu ndani ya Mbao," alisema.
Khamis kwa sasa ana mabao 5 baada ya timu yake kucheza mechi 12, kesho watacheza na timu ya Biashara United katika uwanja wa Karume, Mara.








0 COMMENTS:
Post a Comment