November 2, 2018


Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limesemakuwa, katika uchaguzi wa Yanga, nafasi ambazo zitajazwa ni pamoja na ya mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Manji.

Hayo yamesemwa na Katibu wa BMT, Alex Nkenyenge wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kuelezea mchakato wa Yanga utakavyokuwa.

Manji ambaye kwa muda mrefu amekuwa kiongozi ndani ya Yanga, alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti, lakini wanachama wa Yanga walikataa uamuzi wake huo.

Mbali na wanachama wa Yanga, pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilikuwa halitambui kujiuzulu kwa Manji kitendo ambacho kilitafsiriwa kwamba bado ni mwenyekiti wa Yanga.


2 COMMENTS:

  1. Hivi Yanga aina ubunifu mwingine wa kuifanya kuwa timu bora zaidi ya kumtegemea Yusufu Manji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic