November 17, 2018


Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinatarajiwa kuingia nchini Lesotho leo tayari kwa mchezo wake wa Jumapili dhidi ya wenyeji wao hao kikitokea Afrika Kusini.

Kambi hiyo ya Stars imeno­geshwa na uwepo wa msham­buliaji na nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, am­baye hatashiriki katika mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano lakini atashiriki katika maandalizi yote ya mchezo huo.

Stars iliweka kambi yake nchi Afrika Kusini kwa maandalizi ya siku 10 kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho kwa ajili ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).

Timu hiyo itaondoka Sauz kwa basi kwenda Maseru kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao utakaopigwa siku ya Jumapili.

Kocha Msaidizi wa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema timu inaendelea vizuri na siku ya leo (Ijumaa) itakuwa inaelekea nchini Lesotho.

“Kwa jumla timu inaendelea vizuri na maandalizi yake ya mwisho na leo Alhamisi (jana) tunafanya maz­oezi ya mwisho hapa kisha tunajiandaa kwa safari ya kesho(leo) kwenda Lesotho kwa ajili ya mechi yetu ya Jumapili,” alisema Morocco.

4 COMMENTS:

  1. Tunawatakieni kila la heri na tunawasubiri kuwapokea kwa kishindo

    ReplyDelete
  2. .Mungu atavusha mwaka huu kwenda AFCON

    ReplyDelete
  3. Najivunia Tanzania, najivunia timu yangu ya Taifa, najivunia Bendera ya Taifa langu. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Timu ya Taifa letu; Amina. Tunaamnini Mungu alituandikia 2019 kuwa tutashiriki AFCON.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic