November 16, 2018

Washambuliaji wawili wa timu ya Simba, ambao wamesajiliwa msimu huu, wapo mbioni kuondoka kwa mkopo katika dirisha dogo ambalo limefunguliwa jana.

African Lyon tayari imetuma barua yake ya maombi ili kuweza kupata huduma za wachezaji haoambao ni Marcel Kaheza na Mohamed Rashid kwa ajili ya kuongeza makali yao kwenye safu ya ushambuliaji.

Mohamed Rashid alisajiliwa na Simba akitokea timu ya Prisons na Marcel Kaheza amesajiliwa akitokea timu ya Majimaji ambayo ilishuka daraja.

Tangu wasajiliwe na Simba wamekuwa wakikosa nafasi ya kupata namba ya kudumu kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic