November 16, 2018


Mshambuliaji wa Stand United raia wa Burundi, Alex Kitenge amesema kuwa yupo tayari kuondoka Stand United na kuweza kuitumikia timu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha Mwinyi Zahera.

Kitenge ambaye ni mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga 'hat-trick' amesema kuwa anavutiwa na uwezo wa Ibrahim Ajibu ambaye ni kinara wa kutoa pasi za mwisho za mabao akiwa ametoa 9 mpaka sasa.

"Namkubali Ajibu, anajua kutengeneza nafasi za mabao hivyo ningepata nafasi ya kucheza naye ningefanya maajabu mengi zaidi pia ni jambo jema kupata changamoto mpya kwa sasa hasa kwenye soka la ushindani," alisema.

Kitenge ameshindwa kung'ara baada ya kufunga 'hat-trick' mpaka sasa hajaongeza hata bao moja licha ya kucheza michezo mingine ya ligi kuu hali inayompa wakati mgumu hasa kwa nafasi yake ya ushambuliaji.

1 COMMENTS:

  1. Mwandishi acha uongo kitenge mwenyewe alisema anataka kuchezea simba au kakutuma ili kumtangaza apate ulaji timu kubwa !?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic