November 16, 2018

Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Obrey Chirwa ameanza makeke yake leo katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Chamazi dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 akifunga bao la pili.

Mchezo huu ni wa kwanza kwake tangu asajiliwe katika dirisha dogo akiwa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na timu ya Nogoom ya Misri

Chirwa alionyesha juhudi baada ya kupoke pasi kutoka kwa Yakub Mohamed na kuweza kumsumbua beki kisha akaachia shuti ambalo lilikwenda moja kwa moja kwenye lango la timu ya Taifa ya vijana.

Bao la kwanza la Azam lilifungwa na Enock Atta dakika ya 12 kwa mkwaju wa penati hali iliyofanya timu ya Taifa ya Vijana kushindwa kupata matokeo katika mchezo huo wa kirafiki.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic