November 16, 2018

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho  kitamenyana na timu ya Lesotho katika mchezo wa kutafuta tiketi ya Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) wamepatwa na majanga katika mazoezi hali inayowaweka kwenye hatihati ya kukosa mchezo huo.

Wachezaji hao ambao ni beki Shomari Kapombe na mshambuliaji Rashid Mandawa wanasumbuliwa na majeraha ambayo waliyapata katika maandalizi ya mchezo huo wa marudiano.

Meneja wa timu ya Taifa, Dany Msangi alisema kuwa wachezaji hao wanasumbuliwa na majeraha waliyoyapata wakiwa mazoezini.

"Wachezaji wetu wawili wanasumbuliwa na majeruhi ambayo waliyapata mazoezini ni Kapombe na Mandawa, kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa daktari," alisema.

Stars watacheza Jumapili na timu ya Lesotho ukiwa ni mchezo wa marudio kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic