November 1, 2018






Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limesemakuwa, katika uchaguzi wa Yanga, nafasi ambazo zitajazwa ni pamoja na ya mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Manji.


Hayo yamesemwa na Katibu wa BMT, Alex Nkenyenge wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kuelezea mchakato wa Yanga utakavyokuwa.


Manji ambaye kwa muda mrefu amekuwa kiongozi ndani ya Yanga, alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti, lakini wanachama wa Yanga walikataa uamuzi wake huo.


Mbali na wanachama wa Yanga, pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilikuwa halitambui kujiuzulu kwa Manji kitendo ambacho kilitafsiriwa kwamba bado ni mwenyekiti wa Yanga.


Akizungumzia hilo, Nkenyenge alisema: “Nafasi ya mjumbe wa kamati ya utendaji ama kiongozi ndani ya Yanga, itakoma endapo mtu atafukuzwa au kujiuzulu kwa kuandika barua na kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo, viongozi wengi wa Yanga wamejiuzulu na wengi wameandika barua.


“Miongoni mwao, mwenyekiti pia aliandika barua ya kujiuzulu na hatuna barua nyingine inayoonyesha amerudi kwenye nafasi yake hiyo.


“Juhudi nyingi zilifanyika, sisi tuliwaandikia TFF, TFF walimwandikia Manji barua, lakini haikuishia hapo, waziri alionana naye na kuzungumza naye, kinachoonekana ni kwamba kwa sasa Manji hataki kuwa kiongozi ndani ya Yanga kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano.


“Hivyo sisi kama baraza baada ya kufuatilia yote hayo, katika nafasi ambazo zitaenda kufanyiwa uchaguzi ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti.”

3 COMMENTS:

  1. Uwe unakumbuka ulivyoripoti mwanzo. Tunaanza kuwa na mashaka na uhakika wa habari zako unazoandika.

    ReplyDelete
  2. Mara amerudi Mara amegoma Yan hii blog haina story za ukweli zaidi ya uongo tu,
    Nashangaa watu wanatangaza matangazo yao humu

    ReplyDelete
  3. Nina mashaka na akili za wanaokupa matangazo,maana si kwa habari hizi za hovyo hovyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic