November 2, 2018

Uongozi wa Simba umesema kuwa kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya JKT Tanzania wana kila sababu ya kuweza kuibuka na ushindi kwa kuwa kikosi chao kina uwezo mkubwa.

Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao JKT Tanzania ila hilo haliwafanyi wawe na hofu katika kushindana.

"Sisi ni timu bora kabisa, nasema tuna uwezo mkubwa wa kufanya ushindani, sisi tunatetea ubingwa wetu sio timu ya mchezomchezo.

"Nasema nikiwa na takwimu, tuna piga pasi nyingi sasa mpaka mia, kuna mtu anaitwa Okwi, Bocco, Dilunga, Kagere tunawaheshimu sana JKT pamoja na kuwaheshimu tutafanya makubwa," alisema.

Simba kesho watakuwa ugenini wakicheza dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Mkwakwani uliopo Tanga ikiwa ni mchezo wao wa 10 kwenye Ligi Kuu Bara.

2 COMMENTS:

  1. Acha unyumbu saleh mbn kichwa cha habari akisanifu yaliyomo

    ReplyDelete
  2. USIWE KAMA MASAU BWILE UNAWAPA KAZI WACHEZAJI TAFUTA MANENO YA BUSARA KULINDANA NA KALIA YAKO

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic