Kikosi cha timu ya Coastal Union kilicho chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda kimefanikiwa kupanda kwa kasi ya ajabu kutoka nafasi ya 10 mpaka kufika nafasi ya tano kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Coastal Union ambayo imepanda daraja msimu huu inakuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo kwa timu ambazo zimepanda ligi msimu huu kwa sasa akifuatiwa na JKT Tanzania ambaye yupo nafasi ya sita.
Coatal Union imepanda baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kuwafanya wafanikiwe kuchukua pointi tatu mbele ya Chama la wana.
Katika mchezo mwingine uliochezwa leo, African Lyon wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mabao ya Afrikan Lyon yalipachikwa na Haruna Moshi 'Boban' dakika ya 14 kwa kupiga 'Free-Kick' na bao la pili likafungwa na Kassim Mdoe dk ya 26 na kuwafanya wafanikiwe kuchukua pointi tatu muhimu.
African Lyon kwa sasa wanashika nafasi ya 16 wakipanda kutoka nafasi ya 19 waliyokuwa mwanzo baada ya kufikisha pointi 11 huku Lipuli wakibaki nafasi ya 14 na pointi zao 12.

0 COMMENTS:
Post a Comment