Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga Juma Abdul ambaye amekuwa benchi kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ameambiwa kuwa asahau namba ya kudumu ndani ya kikosi kwa sasa.
Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amesema kuwa amemwambia Abdul kuwa mchezo wao dhidi ya Ndanda FC atapewa namba kutokana na kinda Paul Godfrey kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wao dhidi ya Lipuli FC.
"Nimemwambia Abdul hata acheze kwa kiwango gani katika mchezo wetu dhidi ya Ndanda hawezi kunibadilisha maamuzi yangu ya kumuanzisha Godfrey, nimemwamini na anauwezo mkubwa hivyo anapata nafasi kwa sasa kwa kuwa mbadala wake ana matatizo.
"Siwezi kumuacha Godfrey, ataniuliza anakosea wapi hiyo inakuwa ngumu kwangu na sina namna zaidi ya kumruhusu aanze kikosi cha kwanza, ila kwa kuwa ana kadi nyekundu hatacheza mchezo ujao," alisema.
Juma Abdul amekuwa nje kwa muda msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ambayo aliyapata katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar hali iliyomfanya kocha kumpa nafasi Godfrey ambaye ameanza kuonyesha uwezo wake uliomvutia kocha.

godfrey lazima apate namba kucheza kwa kwa sababu bado ni kijana mdogo ana nguvu ana kasi . ana kila sifa ya kucheza kikosi cha kwanza. juma abdul umri wake ushamtupa kwa nilazima kcha amuandae kurithi hii nuber mbili huyu godfrey
ReplyDeleteTatizo Kocha anaongea sana, hadi sasa anapitiliza. Maneno mengine yanatakiwa yawe ya akiba kwake, kwakuwa yeye ndiye mwenye maamuzi, abaki kuamua tu kuwa leo fulani ndiye anayeanza. Akianza kukosoa madhaifu ya wachezaji wake, mbona kikosi kizima kimeoza, atakosoa wachezaji wote,labda awe na kisa binafsi tu na Abdul.
ReplyDelete