Mshambuliaji wa timu ya Simba Meddie Kagere raia wa Rwanda amefunguka na
kusema kuwa anafanya kazi kwa kujituma na ataendelea kupambana kuhakikisha
anaisaidai timu yake kufanya vizuri na kutaja siri ya kufanikiwa kwake.
Kagere alifanikiwa kufunga mabao 2 ambayo yaliipa pointi tatu Simba mbele
ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga na kufanya
waweze kushinda mchezo wao wa 8 wakiwa na sare mbili na wamepoteza mchezo mmoja
kati ya 11 waliyocheza.
Kagere amesema kuwa anaona fahari
kuisaidia timu yake kushinda ataendelea kufanya hivyo kila anapopata nafasi kwa
kuwa hicho ndicho kimemleta Simba kucheza na kupata matokeo.
"Uwezo wa kusubiri na kuendelea kufanya jambo ingawa ni gumu bila
kulalamika pamoja na nidhamu, kujituma nikiwa ndani na nje ya uwanja kunafanya
niweze kufanya vizuri kila ninapopata nafasi hili ni jambo la kushukuru.
"Ushirikiano uliopo ndani ya timu, pia naamini mwenyewe kile ambacho
nakifanya bila kuwa na hofu ndani ya uwanja, nawapenda sana mashabiki wangu
nawafikiria sana muda mwingi hivyo sina cha kuwambia zaidi ya kuwashkuru kwa
kunikubali pamoja na kunipokea vizuri," alisema.
Kagere anafikisha mabao 7 kwa wafungaji akiwa amefungamana na Emmanuel Okwi
wote wakiwa ni washambuliaji wa kimataifa huku namba moja akiwa ni mzawa Eliud
Ambokile ambaye ana mabao 8.
0 COMMENTS:
Post a Comment