November 5, 2018


Jumla ya wanachama 49 wamempigia kura za hapana mwenyekiti wao mpya Sued Mkwabi  katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere, Posta, Dar es Salaam.

Licha ya wanachama hao kumpa kura ya hapana bado alifanikiwa kupita kwa kishindo kwa kuwa kura nyingi zilionesha kumkubali hali iliyopelekea kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Simba.

Sued Mkwabi alipita bila kuwa na mpinzani baada ya aliyekuwa mshindani wake Mtemi Ramadhani kujiondoa kwenye uchaguzi kutoka na kile alichoeleza kuwa na majukumu mengi na ana mpango wa kuhamia mkoani Dodoma.

Jumla ya wanachama waliopiga kura walikuwa ni 1628 na kura alizopata mgombea Mkwabi ni 1579 huku idaidi ya kura 49 pekee zikiwa hazijamkubali Mwenyekiti huyo mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic