November 8, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa utafanya mazungumzo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumaliza suala la uchaguzi wa klabu hiyo ambao utafanyika Januari mwakani.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaya, amesema wameitwa na TFF kwa ajili ya kufanya mazungumzo ili kufikia mwafaka juu ya suala hilo.

Kaya ameeleza kuwa watakaa kikao na TFF ili kuzungumza kwa undani zaidi hatma ya sakata la kusimamiwa uchaguzi wao jambo ambalo wanachama wamelipinga.

Wanachama wa Yanga waliitisha mkutano juzi kupitia viongozi wa matawi na kupinga suala la kusimamiwa uchaguzi wao na TFF wakisema kila kitu wanapaswa kufanya wao.

Hatua hiyo imechukua sura mpya ambapo sasa TFF imeona iwaite Yanga kwa ajili ya kwenda kukaa kitako kujadili jambo hilo.

1 COMMENTS:

  1. Aaaaaa! Mnaboa bwana! Sasa hayo maagizo ambayo TFF imeyatoa yako wapi! Na je Kichwa cha habari hii uliyoiandika kinaendana na habari iliyopo ndani? Mambo gani haya jamani!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic