November 8, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewacharukia wachezaji wake Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent, Matheo Anthony na Mrisho Ngassa kwa kushindwa kufika mazoezini bila kutoa taarifa, imeelezwa.

Wachezaji hao hawakufika mazoezini juzi ambapo kikosi cha Yanga kinajifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Zahera ameibuka na mkwara wa kusisitiza yeye kama Kocha hatakuwa na mchezaji yoyote ambaye amekuwa hana nidhamu ndani ya timu.

Mkongo huyo amesema haijalishi mchezaji awe na jina kubwa ama ana faida gani katika timu bali atachukua hatua zozote zile kwa atakayekiuka masharti yake.

Yanga wanaendelea kujifua kimazoezi hivi sasa kujiandaa na mchezo ujao wa ligi ambapo watacheza dhidi ya Mwadui FC ugenini.

2 COMMENTS:

  1. Kocha wape adhabu wachezaji wote ambao hawana nidhamu.

    ReplyDelete
  2. Ningekuwa kocha ningeshawapa adhabu bila kupepesa macho,soka bila nidhamu ni sifuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic