Kiungo Papy Tshishimbi sasa yuko katika hali nzuri baada ya kuanza mazoezi na wenzake.
Kiungo huyo raia wa DR Congo alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki kadhaa kutokana na kusumbuliwa na maumivu.
Kukaa kwake nje, kulimfanya Kocha Mwinyi Zahera kuangalia namna nyingine ya kuimarisha kikosi chake.
Hata hivyo, kwa sasa Zahera anaonekana atakuwa na nafasi ya kumtumia katika mechi zinazokuja.
Katika kipindi cha mapumziko ya mechi za kimataifa, Yanga imesafiri hadi mkoanini Lindi kwa ajili ya mechi za kimataifa ili kujiweka vizuri.







Haya ni matatizo makubwa sana ya blog hii! Mwandishi tatizo ni umakini au unazi? Nanukuu ulichokiandika...... "Yanga imesafiri hadi mkoanini Lindi kwa ajili ya mechi za kimataifa ili kujiweka vizuri". Mwisho wa kunukuu. "Mkoanini" tunaweza kusema ni typing error. Ishu inakuja, "Mechi za kimataifa" halafu mkoani Lindi. Hivi hii timu yako ipo katika mechi za kimataifa kweli! Ni ligi gani hiyo wenzetu!. Kuhusu kimataifa kwasasa mnatakiwa kusahau kabisaaaa...
ReplyDelete