November 2, 2018


Na George Mganga

Baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuitaka Yanga kufanya uchaguzi ili kujaza nafasi za viongozi zilizoachwa wazi, uongozi wa klabu hiyo umesema bado haujapata taarifa rasmi.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu, Omar Kaya, ameeleza kuwa wao kama uongozi hawana taarifa hizo, hivyo wanasubiria barua rasmi.

Kaya amegoma kuzungumzia lolote lile mpaka pale barua rasmi itakapofika mezani ndipo klabu itakaa na kuamua jambo la kueleza.

Hata hivyo kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano iliyo chini ya Ofisa Habari, Dismas Ten, jioni ya jana iliarifu kuwa leo klabu itakuwa na kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika majira ya saa 8 za mchana.

Yawezekana kikao hicho kitazungumzia kwa undani juu ya tamko la BMT hivyo tusubiri ili tuje kuona kipi kitajiri.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic