November 30, 2018


Kikosi kizima cha wasanii wanaokwenda kupafom kwenye tamasha la Wasafi kimewasili mjini Iringa na kupata mapokezi makubwa.

Tamasha hilo linafanyika kesho kwenye Uwanja wa Samora mjini hapa na maandalizi yote yamekamilika.

Wasanii hao wakiongozwa na Diamond Platnumz, Harmonize na wasanii wengine kibao wamepokelewa na mashabiki wengi waliokuwa wamejipanga barabarani.

Baada ya mashabiki hao kuwapokea, wasanii hao waliongozana na msafara huo hadi kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ambao aliwaahidi kuwapa ushirikiano wa juu.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic