November 7, 2018


Uongozi wa Yanga kupitia wanachama wake umetishia kuwafikisha Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mahakamani.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tawi la Kariakoo, Kaisi Edwin Kaisi, amefunguka na kueleza hayo jana kupitia Mkutano wa Matawi na kuweka hilo bayana.

Edward alieleza Yanga haiwezi kusimamiwa uchaguzi na TFF kwa kuwa wao wenyewe wanaweza kufanya kila kitu.

Aidha, Edward alieleza kuwa hawaoni shida kuwafikisha BMT na TFF mahakamani kwa kuwa wanaingilia majukumu yao ambayo wanayaweza wenyeji.

BMT iliwataka TFF kusimamia uchaguzi wa Yanga kwa kuwa Kamati yao ya Uchaguzi haijitoshelezi wakiamini ina mapungufu.

3 COMMENTS:

  1. Tukienda mahakamani klabu itafungiwa kucheza mpira tusifanye hivyo. Dawa ni kufanya uchaguzi kwa Yanga wenyewe kujisimamia. Viongozi Yanga njooni na hoja hiyo tuitishe uchaguzi jambo hili tulimalize vyema.

    ReplyDelete
  2. yanga fanyeni uchaguzi matatizo mengine mnayataka wenyewe kwani uongozi muda umeshapita pia viongozi wamejiuzulu nyie bado mnawang'ang'ania acheni uzuzu timu yenyewe hamuichangii mnabaki kupiga domo

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe hujitambui,sio kosa lako ni konki konki konki

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic