November 7, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi Yanga Tanzania, Bakili Makele, amesema leo ataenda katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) kueleza kwanini amepinga klabu hiyo kusimamiwa uchaguzi wake na shirikisho.

Kamati ya Maandili ya TFF imemuita Makele kwenda kueleza hoja za msingi za kupinga suala hilo baada ya kupewa maagizo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Makele amekuwa mmoja wa viongozi na wanachama Yanga wanaopinga maamuzi ya BMT kuitaka TFF isimamie uchaguzi wa klabu yao wakisema haina kamati inayojitosheleza.

Hata hivyo Makele amefunguka na kusema hajaona sababu ya msingi ya kuitwa TFF akieleza hoja walizompatia akajieleze hazina mashiko hivyo ataenda kutimiza wajibu.

Makele bado ameonekana kuwa na msimamo wa kuungana na wanachama wenzake kupinga kwa uzito juu ya TFF kutaka iisimamie Yanga uchaguzi wake ambao umepangwa kufanyika Januari 1 2019.

1 COMMENTS:

  1. TFF mchukulieni hatua kali huyu .. Mfungilieni mbali ..asijihusishe na mpira maisha ...huyo anayepinga jambo la manufaa kwa klabu na nchi kwa ujumla

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic