November 10, 2018


Zikiwa zimebaki siku tano, dirisha dogo la usajili kufunguliwa,uongozi wa timu ya Yanga umesema kuwa utatumia nafasi hiyo kufanya usajili kwa kuzingatia ripoti ya kocha ambaye alisema anataka kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Yanga, Hussen Nyika amewataka mashabiki wa Yanga watulie kwa kuwa kamati imejipanga kuhakikisha inafanya kazi yake kwa umakini bila kukurupuka.

"Bado dirisha la usajili halijafunguliwa hivyo nasi tunatambua kuwa kuna uhitaji wa kufanya hivyo, tunachosubiri ni ripoti kutoka kwa kocha mkuu ili tujue tunasajili mchezaji gani, mipango ipo sawa," alisema.

Kocha Mkuu Mwinyi Zahera, alieleza kuwa amewachunguza wachezaji wa kimataifa watatu ambao ni kutoka Ghana,Ghaboni na Congo hivyo makubaliano yakiwa sawa huenda wakatua nchini kuitumikia Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Mwaka Jana tulisubiri hivyo hivyo mwisho mkatuletea kindoki, goalkeeper anayezidiwa hata na kabwili. Hussein nyika kazi imekushinda mzee wa 10%

    ReplyDelete
  2. Mwaka Jana tulisubiri hivyo hivyo mwisho mkatuletea kindoki, goalkeeper anayezidiwa hata na kabwili. Hussein nyika kazi imekushinda mzee wa 10%

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic